Dennis Oliech
Timu ya
Taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars, imekwama mjini Khartoum, baada ya
kuwasili kwa mchuano wa kimataifa wa kirafiki na wenyeji wao Sudan.
Ripoti zinasema kuwa aliyekuwa kocha
wa Kenya na mshambulizi wa Ajaccio Dennis Oliech, ametuma ujumbe kwenye
ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii Facebook, kulalamikia waandalizi wa
mechi hiyo, ambayo imeratibiwa kuchezwa hii leo.Oliech amelalamika kuwa hawajui mahala ambapo mechi hiyo itachezwa.
''Sasa ni saa tano za mchana na tunasikia tu kuwa tungali na safari ya masaa mawili kabla ya kufika uwanjani na hata hawatuambii ni wapi'' Alisema Oliech.
Kabla ya stars kuondoka, shirikisho la mchezo wa soka nchini Kenya, lilisema kuwa mechi hiyo itachezwa leo mjini El Fasher.
Timu hiyo iliondoka nairobi siku ya jumanne kuelekea Khartoum huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuandikisha ushindi.
Wachezaji watatu wa kulipwa, Dennis Oliech, David Ochieng na Victor Wanyama ni miongoni mwa waliosafiri.
Harambee stars wamepangiwa kucheza na timu ya taifa ya Namibia katika mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka huu mjini Nairobi.
Hata hivyo mechi hiyo haitakuwa na maana yoyote kwa kuwa timu hizo mbili tayari zimeondolewa kwenye fainali za mwaka huu.
Kocha wa Harambee Stars Adel Amrouche hakusafiri na timu hiyo kwa kuwa hajarejea mjini Nairobi, tangu alipoenda likizoni Desemba mwaka uliopita.
0 comments:
Post a Comment