Recent Posts

Tuesday, March 11, 2014

Atl. Madrid 4 - 1 Ac Milan (Agg 5-1)

Atletico Madrid: Courtois, Juanfran, Miranda, Godin, Filipe Luis, Turan (Rodriguez 78), Gabi, Mario Suarez, Koke (Diego 81), Raul Garcia (Sosa 72), Diego Costa.
Subs Not Used: Aranzubia, Villa, Alderweireld, Insua.
Booked: Raul Garcia.
Goals: Diego Costa 3, 85, Turan 40, Raul Garcia 71.

AC Milan: Abbiati, Abate, Rami, Bonera, Emanuelson, Essien (Pazzini 68), Poli, De Jong (Muntari 78), Kaka, Taarabt (Robinho 46), Balotelli.
Subs Not Used: Amelia, De Sciglio, Mexes, Zaccardo.
Booked: Rami, Balotelli, Bonera, Robinho.
Goals: Kaka 27.
Att: 55,000.
March: Diego Costa scored two goals as Atletico moved through to the last eight of the Champions League

Bayern Munich 1 - 1 Arsenal (Agg 3 - 1)

Bayern Munich: Neuer 6; Lahm 7, Javi Martinez 7, Dante 6, Alaba 6; Schweinsteiger 7, Alcantara 6.5; Robben 6.5, Gotze 6 (Kroos 59, 7), Ribery 6.5; Mandzukic 6.
Subs: Starke, van Buyten, Rafinha, Pizarro, Boateng, Muller.
Booked: Dante.
Manager: Pep Guardiola 6.5.
Goals: Schweinsteiger 54

Arsenal: Fabianski 7; Sagna 6.5, Mertesacker 7, Koscielny 7, Vermaelen 6.5; Arteta 6, Oxlade-Chamberlain 7.5; Cazorla 6.5, Ozil 4 (Rosicky 46, 6), Podolski 7; Giroud 6.5.
Subs: Viviano, Jenkinson, Flamini, Gnabry, Hayden.
Booked: Podolski, Arteta.
Manager: Arsene Wenger 6.5.
Goals: Podolski 57
Progressing together: Bayern players celebrate as a team after going ahead on the night at the Allianz

KOCHA MANUEL PELLEGRINI AWAONGOZA MAN CITY KUELEKEA SPAIN, TAYARI KWA MARUDIANO NA BARCA KWENYE UEFA CHAMPIONS LIGI.


Calm: The Manchester City boss looked relaxed despite the side facing an early exit
Kocha wa Man City Manuel Pellegrini na kikosi chake wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa  Manchester tayari kwa kuruka kuelekea Spain kucheza kipute na  Barcelona, Kumbuka ni Marudiano ya UEFA Champions Ligi.

Kikosi cha  Manchester City kwenye Uwanja wa Ndege tayari kwa kuruka Spain,  Samir Nasri, Yaya Toure, Vincent Kompany ana Sergio Aguero wamo ndani kwenye safari hiyo kwenda Spain.
Best chance: Spaniards Alvaro Negredo and David Silva will hope to make an impact on home soilDowncast: Right back Pablo Zabaleta drags his suitcase into the airport as he considers mission impossible
Pablo Zabaleta, Alvaro Negredo na David Silva kuongeza kasi kesho jumatano ili waweze kupindua mabao 2-0 ambayo walifungwa wakiwa kwao Etihad kwenye mechi ya raundi ya kwanza.

Up close and personal: Costel Pantilimon will be in Spain as Hart's back-up
Keeping options: Joe Hart needs to keep a cool head going into the Champions League tie
Makipa wote wawili Joe Hart na Costel Pantilimon ndani dhidi ya Barcelona.

BASI LA HOOD KUTOKA ARUSHA - MBEYA LAPATA AJALI SAME,KILIMANJARO

 

 
Basi la Kampuni ya Hood likiwa limepinduka na watu kuumia vibaya Same,Kilimanjaro chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana. 
Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo

BAADA YA KUFANYA NGOMA NA MOVIE, MSANII NAJ AKWEA PIPA KUELEA NCHINI UINGEREZA


 
Mwanamuziki wa muziki wa Bongo Fleva,Naj,Jumamosi iliyopita aliachia ngoma yake aliyomshirikisha Dogo Aslay, lakini siku iliyofata Naj alisepa kuelekea nchini Uingereza ambako ndiyo anapoishi baada ya kumaliza masomo yake
. 
Naj alikuwepo nchini kwa miezi kadhaa na kufanya projects nyingi ikiwemo movie ambayo yeye mwenyewe ndiyo exucutive producer, na ndani ya hiyo movie kuna mastaa kibao wa bongo flava na bongo movie
Clouds fm imepiga stori na Naj akafunguka jinsi atakavyoweza kufanya game na wakati huo huo akipiga kazi nchini Uingereza.
Pamoja na hayo Naj akazungumzia uhusiano wake wa kimapenzi baada ya kuachana na Mr Blue ambaye walikuwa pamoja kwa muda wa miaka miaka mitano, na ndiye aliyemmwaga Naj na kuendelea na baby mama wake, je tangu mwaka juzi hadi leo Naj ameshapata new boyfriend?

Sunday, March 9, 2014

TAIFA STARS KUTUMIA JEZI ZA ADIDAS



1group_200da.jpg
Hizi ndiyo Jezi mpya za Adidas za Taifa Stars
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilifikia makubaliano na kampuni ya Adidas kupitia msaada wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya michezo.
Kufuatia makubaliano hayo TFF tulipatiwa vifaa kadhaa vya adiads kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars). Vifaa hivyo zikiwemo jezi tulianza kuvitumia kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek.
Vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.
TFF tunaishukuru kampuni ya Adidas ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa miaka mingi kwa mchango wao huu wa kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Boniface Wambura Mgoyo

Rwanda yafukuza afisa wa Afrika Kusini



news002px_c439f.jpg
Waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Rwanda amethibitisha kuwa serikali inawafukuza maafisa sita wa ubalozi wa Afrika Kusini, saa chache baada ya Afrika Kusini kuwataka raia watatu wa Rwanda kuondoka nchini humo.
Afrika Kusini ilichukua hatua hiyo baada ya nyumba ya mpinzani mmoja wa Rwanda anayeishi Afrika Kusini kushambiliwa siku ya Jumaane.
Jenerali Kayumba Nyamwasa, ambaye aliwahi kuwa mkuu wa majeshi nchini Rwanda, hakuwa nyumbani wakati wa shambulio hilo.
Nyumba yake iliharibiwa na komputa na baadhi ya nyaraka zilichukuliwa.
Jenerali Nyamwasa amenusurika na majaribio mawili mengine ya kumuuwa akiwa Afrika Kusini.
Tayari watu wanafanyiwa kesi ya kujaribu kumuuwa - wakiwemo Wanyarwanda watatu na Watanzania watatu.(P.T)

MAMBO YA JANA CHELSEA 4 v TOTTENHAM

Wachezaji wa Chelsea wakipongezana baada ya kufunga bao la nne na la mwisho, Bao mbili zikifungwa na Demba Ba katika dakika za mwishoni na ndani ya muda mfupi. Chelsea wameshinda bao 4-0. Ushindi huu ukiwaweka Kileleni zaidi kwa kupata pointi 66.
Eden Hazard akishangilia bao lake la mkwaju wa penati katika dsakika ya 60 kipindi cha pili baada ya Eto'o kuangushwa ndani ya 18 (ndani ya box) eneo hatari..Sense of humour: Eto'o aims his celebration at those saying he is too old for the Chelsea team
.

Kipindi cha pili dakika ya 56 Samwel Eto'o aliipatia bao safi baada ya kuwachomoka mabeki wa Spurs na kumfunga kipa wa Spurs. Dakika ya 60 mchezaji huyo huyo Eto'o ameangushwa kwa kufanyiwa rafu mbaya na Mchezaji wa Spurs Kaboul na mwamuzi wa mtanange huo Michael Oliver kumtoa kwa kadi nyekundu na mkwaju wa penati kutengwa kwenda lango la Spurs. Dakika za mwishoni dakika ya 88 na dakika ya 89 Demba Ba ameifungia timu yake Chelsea bao mbili za haraka! Bao la pili akilifunga dakika ya 89 baada ya Mchezaji wa Spurs kurudisha mpira nyuma kwa kichwa na hatimae Demba Ba kuwa kuwa karibu na kipa huyo na kumzunguka na kuupata mpira huo na kumfunga kipa wa Spurs bao hizo mbili za haraka na kwenye muda wa dakika za lala salama! Ushindi huu unawasogeza kileleni zaidi Chelsea kwa kufikisha pointi 66 wakifatiwa na Liverpool wenye alama 59.Hazard ndie aliyeutokomeza mkwaju huo ndani ya lango la Spurs na kufanya Chelsea wanaochezea kwenye uwanja wao wa Stamford Bridge kuongoza kwa bao 2-0.
Kipindi cha kwanza kilimalizika 0-0 
Samuel Eto'o akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza kwa timu yake Chelsea.....' Meneja wa Chelsea Jose MourinhoAnimated: Chelsea boss Jose Mourinho gesticulates from the touchline during the game!Mchezaji wa Chelsea Eden Hazard akikosa bao la wazi hapa huku kipa wa Spurs  Hugo Lloris akiwa nje ya lango lake.!!..
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Lampard (Oscar 46), Matic, Ramires, Hazard, Schurrle, Eto'o.
Subs: Mikel, Ba, Willian, Schwarzer, Kalas, Salah.
Booked: Lampard.
Goal: Eto'o 56, Hazard pen 60.
Tottenham: Lloris, Naughton, Dawson, Kaboul, Vertonghen, Sandro, Bentaleb, Walker, Sigurdsson (Paulinho 61), Lennon, Adebayor.
Subs: Soldado, Townsend, Chadli, Friedel, Fryers, Kane.
Booked: Bentaleb, Naughton, Sandro.
Sent off: Kaboul.
Referee: Michael Oliver

Wednesday, March 5, 2014

Harambee Stars wakwama Khartoum

Dennis-Oliech-risks_79da1.jpg
Dennis Oliech
Timu ya Taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars, imekwama mjini Khartoum, baada ya kuwasili kwa mchuano wa kimataifa wa kirafiki na wenyeji wao Sudan.
Ripoti zinasema kuwa aliyekuwa kocha wa Kenya na mshambulizi wa Ajaccio Dennis Oliech, ametuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii Facebook, kulalamikia waandalizi wa mechi hiyo, ambayo imeratibiwa kuchezwa hii leo.
Oliech amelalamika kuwa hawajui mahala ambapo mechi hiyo itachezwa.

''Sasa ni saa tano za mchana na tunasikia tu kuwa tungali na safari ya masaa mawili kabla ya kufika uwanjani na hata hawatuambii ni wapi'' Alisema Oliech.
Kabla ya stars kuondoka, shirikisho la mchezo wa soka nchini Kenya, lilisema kuwa mechi hiyo itachezwa leo mjini El Fasher.
Timu hiyo iliondoka nairobi siku ya jumanne kuelekea Khartoum huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuandikisha ushindi.
Wachezaji watatu wa kulipwa, Dennis Oliech, David Ochieng na Victor Wanyama ni miongoni mwa waliosafiri.
Harambee stars wamepangiwa kucheza na timu ya taifa ya Namibia katika mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka huu mjini Nairobi.
Hata hivyo mechi hiyo haitakuwa na maana yoyote kwa kuwa timu hizo mbili tayari zimeondolewa kwenye fainali za mwaka huu.
Kocha wa Harambee Stars Adel Amrouche hakusafiri na timu hiyo kwa kuwa hajarejea mjini Nairobi, tangu alipoenda likizoni Desemba mwaka uliopita.

Carles Puyol kuhama Barcelona



carles-puyol.1_c088f.jpg
Carles Puyol.
Nahodha wa klabu ya Barcelona Carles Puyol ametangaza atawahama mabingwa hao wa Hispania mwishoni mwa msimu huu.
Puyol mwenye umri wa miaka 35 aliibukia kutoka vikosi vya vijana wa Barcelona na kujiunga na kikosi kikuu mwaka 1999, amewachezea mabingwa watetezi wa La Liga takriban mara 400.
Ameshinda vikombe sita vya ubingwa wa Ligi,vikombe vitatu vya klabu bingwa ya Ulaya,vikombe viwili vya shirikisho la kandanda la Uhispania pamoja na vikombe vya super cup vya klabu za ulaya na Uhispania, pia amekua mchezaj muhimu katika nyanja ya kimataifa akiisaidia Hispania kunyakua ubingwa wa bara la Ulaya mwaka 2008 na kombe la dunia miaka miwili badae.
Hata hivyo amekua akisumbuliwa na magoti katika miaka ya hivi karibuni na hakuweza kushiriki katika michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2012, msimu huu ameichezea Barcelona mara 12 tu.
Puyol, ambae ameiwakilisha Hispania mara 100,alicheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Uruguay, Februari 2013, amesema angependa kupumzika baada ya kuondoka Barcelona. "sijui ntakachofanya baada ya Juni 30 lakini nina hakika nitapumzika" akaongeza. "nitaitisha mkutano na waandishi habari mwishoni mwa msimu huu ili niwaage baada ya kuichezea klabu hii kwa muda wa miaka 19 ," alisema Puyol.

RIDHIWANI AMWANGUSHA MADEGA KWENYE KURA ZA MAONI HUKO CHALINZE!


 




Kuelekea uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani lililoachwa wazi baada ya mbunge wake SAID BWANAMDOGO kufariki hivi karibuni Chama cha Mapinduzi kimefanya kura ya maoni ili kumpata mrithi wa Jimbo hilo atakayechuana na wagombea kutoka vyama vingine.



Katika kura hiyo ya maoni wagombea watatu wamejitokeza kuwania nafasi ya ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia chama cha CCM akiwemo mbunge wa zamani wa Jimbo hilo RAMADHAN MANENO, mwenyekiti wa zamani wa Yanga IMANI MADEGA na mdau mkubwa wa soka hapa nchini na mwanachama wa Yanga RIDHIWANI KIKWETE.
Baada ya kura kupigwa RIDHIWANI KIKWETE ndiye amepata Baraka za wanaCCM kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge kwa kumpa kura 758 huku IMANI MADEGA akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 335 na RAMADHAN MANENO akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 206.

 

Jiunge na Jamii Yetu

Wasiliana nasi

Barua pepe: dennybazira@gmail.com

Timu Yetu